Nội dung text Kuwasiliana kwa njia ya mazungumzo Topic 6 - WazaElimu.com.pdf
1 SURA YA SITA Kuwasiliana kwa njia ya mazungumzo Dhana ya Mazungumzo. Mazungumzo ni utaratibu wa kuongea baina ya pande mbili ambapo wahusika wa mazungumzo hayo huwa ni watu. Kwa kawaida mazungumzo huwasilishwa kwa njia ya mdomo na huweza kuambatana na ishara za viungo vya mwili. Chanzo cha mazungumzo huwa ni mzungumzaji na kikomo chake huwa ni msikilizaji. Mzungumzaji huwa ni mtu anayeanzisha uneni, huyu kifasihi huitwa fanani. Uneni ni utoaji wa matamko yenye maana katika lugha fulani ilihali kitendo ni dhana ya utendaji . Msikilizaji huwa ni mtu anayepokea uneni kutoka kwa mzungumzaji huyu kifasihi huitwa hadhira. Misingi ya Mazungumzo Ili watu waweze kuelewana vizuri wanapozungumza ni lazima wazingatie mambo makuu yafuatayo,Pia mambo hayo yasipozingatiwa yanaweza kuathiri mazungumzo ya wazungumzaj (i) Uhusiano wa wazungumzaji Unaweza kuelewa na kutambua uhusiano wa watu wanaozungumza kama ni marafiki , wapenzi, baba na mtoto au mwalimu na mwanafunzi watu au wazungumzaji ni maadui kwa kuangalia msamiati wanayotumia katika mazungumzo yao. Msamiati wanayotumia katika mazungumzo yao. Msamiati anayotumia mwalimu na mwanafunzi wake ni tofauti sana na msamiati anayotumia mtoto na wazazi wake kwa sababu , msamiati utakaotumika na mwalimu na mwanafunzi wake hutawaliwa na heshima busara na ulezi zaidi tofauti na msamiati utakaotumika na mtoto na wazazi wake kwani yenyewe hatawaliwa na madoido, madokezo na mabembelezo zaidi. (ii) Mada inayozungumzwa Mazungumzo hutawaliwa na mada , mazunguzumo huhusisha mada inayozungumzwa ambayo pia huamua msamiati kwa kutumia katika mazungumzo husika. Kwa mfano mada inaweza kuwa siasa, masomo, sherehe au muziki. Wazungumziaji wana takiwa kuchagua msamiati kulingana na mada. Kwa mfano mada ya masomo inaweza kuibua msamiati kama vile elimu, itifaki. (iii) Muktadha wa Mazungumzo Mazungumzo huathiriwa na miktadha tofauti tofauti muktadha wa mazungumzo unaweza kuwa rasmi au usiwe rasmi, kuna miktadha mbalimbali ambayo wazungumziaji huweza kutumia wakati wa mazungumzo yao. Miktadha kama hiyo ni shuleni, dukani, mjini, barabarani, kijijini n.k . Kwa mfano , lugha anayotumia daktari hospitalini ni tofauti na lugha anayotumia daktari huyohuyo akiwa nyumbani kwake hivyo lugha hutofautisha kulingana na muktadha wazungumzaji wanapaswa kuzingatia muktadha wa mazungumzo yao. Mfano.
2 Mazungumzo ya mama na mwanae wakiwa kwenye daladala. MTOTO:Mama , mbona kila siku baba anakupiga? MAMA:Chukua andazi mwanangu. Kwa mfano huu, Mama amezingatia muktadha ndio maana hahitaji mazungumzo yaendelee , kwani mada husika haifai kuzungumziwa kwenye daladala (iv) Lengo la mazungumzo Mzungumzaji huwa na lengo la kuzungumza anapokutana na mwenzake ili kukidhi lengo la mazungumzo, mzungumzaji huhitaji kutoa ufafanuzi wa yale anayoyasema ili msikilizaji aelewe kama ilivyokusudiwa . Lengo la mazungumzo linaweza kuwa kutoa taarifa , kuhoji, kukejeli ,kuelimisha ,kuonya au kutia moyo. (v) Muda /wakati wa mazungumzo Mzungumzaji ni lazima ateue msamiati utakaoendana na wakati katika eneo husika . Matumizi mabaya ya muda katika eneo amabalo si rafiki hufanya mazungumzo kuchosha. (vi) Utanzu au aina ya mawasiliano Kabla ya mazungumzo , mzungumziaji ni lazima ajiulize kwamba ujumbe aliokusudia kufikisha kwa hadhira ataufikisha kwa mbinu ipi? Mbinu ya majadiliano, masimulizi, hotuba au nyimbo. (vii) Shughuli inayofanyika Msamiati unaotumika katika mazungumzo huendana na shughuli inayohusika kwa mfano kama shughuli inayofanyika ni ufugaji , uchimbaji madini na msamiati wake utaendana na shughuli husika. Mifano ifuatayo inaonesha mazungumzo katika miktadha tofauti. Mfano 1 Mazungumzo ya kanisani MCHUNGAJI: Bwana Yesu apewe sifa WAUMINI: Amina MCHUNGAJI: Naomba mfungue biblia zenu. Mfano 2 Mazungumzo ya marafiki. BAHATI: Mambo sanura? SANURA: Poa tu vipi wewe? BAHATI :Fresh rafiki yangu, vipi jana mama hakukutia ndimu ulipochelewa kurudi? SANURA: Loo! Mama Yule na ule mdomo wake, alinichimba biti sana. Mfano 3. Mazungumzo ya shuleni
3 MWANAFUNZI:Shikamoo mwalimu MWALIMU: Marahaba , hujambo? MWANAFUNZI: Sijambo (viii) Hali za wahusika wakati wa mazungumzo Lugha inayotumika inapaswa kuendana na hali za wahusika wakati wa mazungumzo ili kuleta maelewano . kwa mfano kama mzungumzaji ni mgonjwa au amekasirika, lugha inayotumika kuwasiliana naye itaendana na hali hiyo. ZOEZI Hatua za kufanya mazungumzo katika lugha ya kiswahiliKatika kufanya mazungumzo zipo hatua mbalimbali za kufuata wazungumzaji wanapokutana kuzungumza , Hatua hizo ni hizi zifuatazo; Salamu Watu wawili wanapokutana kuzungumza sharti wasalimiane kabla ya kuanza mazungumzo hayo, Jambo la kwanza huwa ni salamu, salamu hii huwa rasmi au isiyo rasmi kutegemea na uhusiano uliopo baina ya wazungumzaji , Salamu rasmi inaweza kuwa kama ifuatavyo; Habari za asubuhi na habari za kazi, Salamu zisizo rasmi inaweza kuwa hujambo? Mambo, vipi hali yako, kumbuka kuwa “kwa heri “ siyo salamu. Utambulisho Wazungumzaji wanapokutana wana nafasi ya kutambuana . kipengele hiki hufanyika mara baada ya wahusika kusalimiana katika utambulisho wazungumzaji hutaja majina yao na wasifu wao kwa ujumla. Kwa mfano, unaitwa nani, wewe ni nani?. Hii huwasaidia wazungumzaji kujenga mipaka, uhusiano na mazoea , ukimtambua mtu unayezungumza naye itakupa urahisi wa kuchagua msamiati utakaotumia unapozungumza naye. Andaa mazungumzo yanayoweza kuzungumzwa katika maeneo yafuatayo; a) Hospitalini b) stendi ya mabasi c) Dukani d) Sokoni e) Shuleni
4 Mazungumzo mafupi Mara baada ya utambulisho , wazungumzaji hufanya mazungumzo mafupi kwa nia ya kutaka dhima ya mazungumzo yao. Mazungumzo kamili Mazungumzo kamili hutegemea muktadha, lengo la mazungumzo , mada ya mazungmzo na uhusiano uliopo baina ya wazungumzaji . Ni sehemu hii ambayo hutumia muda mrefu wakati wa mazungumzo. Ufafanuzi Ni kipengele kinachohusu mambo yote ambayo hayakueleweka kwa mmoja kati ya wazungumzaji ,hivyo kurudiwa na kutolewa maelezo ya ziada. Kukatisha Mazungumzo Kipengele hiki ni muhimu sana wakati wa mazungumzo, mathalani umetembelewa na ndugu yako ofisini kwako, kwa bahati mbaya ndugu yako huyo anaongea sana kiasi kwamba wageni wengine wanalalamika nje ya ofisi inakupasa ukatishe mazungumzo . zipo njia mbalimbali za kukatisha mazungumzo mfano, kama umekaa kwenye kiti unaweza kusimama kisha kumsogelea na kumpa mkono mtu unayezungumza naye ukaongea naye kwa maneno kama vile “Nitakushukuru, karibu tena, tuonane wakati mwingine n.k Kuagana Tumia maneno kulingana na muktadha mfano kama ni ofisini waweza kutumia maneno rasmi kama vile “Nakutakia kazi njema, kila la kheri , tuonane wakati mwingine na unaweza kutumia maneno kama vile baadaye furahia siku yako katika muktadha usio rasmi. Lugha fasaha Lugha fasaha ni ile ambayo inafuata taratibu zote za lugha hiyo ikizingatia maana, matamshi, muundo na mantiki. Lugha inapotumika vibaya huweza kupotosha lengo la mzungumzaji. Makosa haya yanaweza kujitokeza katika msamiati (maana) miundo, matamshi na mantiki. Kwa mfano, Kurara, neno hili si neno fasaha kwa sababu katika lugha ya Kiswahili hutamkwa kulala. Ili mazungumzo yaweze kuwa mazuri, wazungumzaji lazima watumie lugha kwa ufasaha. Angalia makosa mbalimbali ambayo huweza kufanywa na watumiaji wa lugha fasaha