PDF Google Drive Downloader v1.1


Báo lỗi sự cố

Nội dung text Kusoma kwa Ufasaha na Ufahamu Topic 5 - WazaElimu.com.pdf

SURA YA TANO Kusoma kwa Ufasaha na Ufahamu Kusoma kwa ufasaha ni kusoma matini kwa usahihi kwa kuzingatia taratibu za uandishi. Mambo ya kuzingatia katika kusoma kwa ufasaha. a) Matamshi sahihi ya maneno. b) Alama za uandishi c) Kasi stahiki d) Mtiririko wa aya e) Utamkaji sahihi wa silabi zenye mkazo na kiimbo katika maneno ilikupata maana sahihi Kusoma kwa Ufahamu Kusoma kwa ufahamu ni uwezo wa kusoma na kuelewa jambo fulani liliandikwa. mtu anaweza kupata ufahamu kutokana na kusoma kifungu cha habari, makala, kitabu au gazeti. Mambo ya kuzingatia katika kusoma kwa ufahamu a) Kusoma matini kwa sauti au kimya b) Kurudia kusoma matini hiyo kwa makini na kubainisha mambo ya msingi yaliyomo katika matini hayo. c) Kuwa makini katika kutafakari jambo alilolisoma ili aweze kutoa taarifa iliyo sahihi au kujibu maswali kwa usahihi. d) Msomaji anatakiwa kufahamu matini anayoisoma inahusu nini e) Msomaji anatakiwa kubaini maneno mapya yaliyotumika katika matini aliyoisoma na namna yalivyotumika ili kutambua lengo la mwandishi. Umuhimu wa kusoma kwa ufasaha na ufahamu a) Huwezesha kukuza uelewa wa mambo mbalimbali na stadi za kuzungumza na kuandika b) Kukuza uwezo wa kujenga hoja juu ya mambo mbalimbali na kujieleza kwa ufasaha na kwa ufupi. c) Hukuza uwezo wa kuchambua mambo anuai na kuchochea ari ya kujisomea. Dhana ya ufahamu. Ufahamu ni neno linalotokana na neno kufahamu. Kufahamu ni kuwa na taarifa sahihi na za kutosha juu ya jambo au tukio fulani kiasi cha kuweza kulifafanua kwa mtu mwingine naye akaelewa. Ni ile hali ya kujua na kuelewa jambo kwa undani na kuweza kulifafanua au kulitolea taarifa. Tunaweza kupima kuwa mtu fulani ana ufahamu kutokana na uwezo wake wa kufafanua jambo Fulani kwa undani Zaidi. Ufahamu hutokana na kuona au kusikiliza. Umuhimu wa ufahamu Ufahamu ni kipengele muhimu sana katika taaluma ya lugha kwa sababu zifuatazo; a) Huwezesha kukuza uelewa wa mambo mbalimbali b) Husaidia kukuza uwezo wa kujenga hoja
c) Husaidia uwezo wa kuchambua mambo d) Huchochea hali ya kujifunza mambo mbalimbali e) Husaidia kuwa na uwezo wa kujieleza kwa ufupi na kwa ufasaha Dhima ya ufahamu. Ufahamu una dhima mbalimbali katika Maisha ya kila siku. Miongoni mwa dhima hizo ni Pamoja na hizi zifuatazo; a) Huokoa muda kwa kutoa taarifa mbalimbali kwa muhtasari. Kufahamu jambo kwa undani kunasaidia mtu kulielezea jambo hilo kwa muhtasari ili kuokoa muda tofauti na asiyefahamu jambo hilo ambaye anaweza kuelezea jambo hilo kwa muda mrefu. b) Kuelimisha. Mtu anaposoma habari fulani akaielewa bila shaka huelimika kutokana na alichokisoma. Hujipatia elimu na maarifa yaliyomo katika kifungu hicho. Kwa mfano kusimulia mwenzake hadithi aliyosoma au tukio aliloliona kunaweza kumfanya abadilike. c) Huokoa gharama Mtu anayefahamu jambo lakini akaweza kulielezea jambo hilo kwa ufupi bila shaka huokoa gharama. Kwa mfano unaweza kuandika barua kwa kutumia karatasi moja tu badala ya kutoa maelezo mengi katika karatasi mbili au tatu. d) Hukuza lugha Msomaji anaposoma habari humjenga na kujiongezea maneno au msamiati mpya wakati mwingine ambao hujawahi kuusikia au kuutumia. e) Huongeza maarifa Kusoma vitabu ni Zaidi ya kusafiri na kwenda nchi ambayo hujawahi kufika. Ndani ya maandishi kuna ushauri, kuna Faraja na maarifa mbalimbali ambayo yanatokana na uzoefu wa Maisha ya mwandishi. Aina za ufahamu Kuna aina tatu za ufahamu, yaani ufahamu wa kuona, kusikiliza na kusoma. Aina y ufahamu hutegemea njia aitumiayo mtu kupata taarifa. a) Ufahamu wa kuona Ni aina ya ufahamu unaohusu kutazama vitu au matukio na kuyatafakari kwa lengo la kupata ujumbe. Ufahamu huu huhusisha namna mtu anavyoweza kutazama matukio mbalimbali kisha kuweza kusimulia matukio hayo kwa wengine. Mfano, mtu aliyetazama mchezo wa mpira wa miguu uwanja wa Taifa kisha kuwasimulia wenzake. b) Ufahamu wa kusikiliza

(e) Kuzingatia kanuni za lugha husika kama vile matamshi (ii) Ufahamu wa kusoma kimya Ufahamu wa kusoma kwa kimya ni ufahamu wa kusoma habari pasipo kutamka maneno kwa sauti inayosikika. Msomaji hupitisha macho kwa kwa haraka katika kila mstari wa maandishi akiwa amefumba kinywa chake. Usomaji wa aina hii hutumika sana maktaba sehemu ambako watu hawaruhusiwi kujadiliana wala kuongea. Ni aina ya usomaji Rafiki kwa watu wanaojiandaa kwa mitihani. (iii) Ufahamu wa kusoma kwa makini Ufahamu wa kusoma kwa makini ni aina ya usomaji ambao msomaji huvuta fikra aina hii ya ufahamu. Aina ya maswali ya ufahamu Ili kujua kwamba kilichosomwa kimeeleweka msomaji hupewa maswali akijibu kwa urahisi huonesha kuwa ameelewa na akijibu vibaya huonesha kuwa hakuelewa. Zipo aina mbili za maswali yanayoulizwa mara kwa mara kutokana na habari ya ufahamu. Aina hihi ni zifuatazo: (a) Maswali mafupi Ni aina ya maswali yanayohiaji majibu mafupi mafupi. Maswali hayo ni kama vile: (i) Maswali ya ndiyo kwa sentensi zilizo zilizo sahihi na hapana kwa sentensi zisizo sahihi. Wakati mwingine maswali haya huliza kama ni kweli kwa sentensi zilizo sahihi na si kweli kwa sentensi zisizo sahihi. (ii) Maswali ya kuchagua jibu lililo sahihi kutoka kwenye orodha ya majibu. (iii) Maswali ya kukamilisha majibu kwenye sehemu zilizoachwa wazi (iv) Maswali ya kuoainisha neno au kifungu kimoja na neno au kifungu kingine ili kuleta maana iliyo sahihi (b) Maswali marefu Ni aina ya maswali ambayo yanamhitaji msomaji afafanue jibu kwa kutumia busara yake. Maswali ya aina hii humtaka msomaji atoe Ushahidi au uthibitisho wa mawazo yake juu ya kile anachojibu. Mbinu za kujibu maswali yatokanayo na habari. a) Kuvuta makini na kusikiliza bila kuruhusu kuingiliwa na mawazo mengine. b) Kusikiliza au kusoma habari yote kwa makini c) Kusikiliza au kusoma kila swali kwa makini d) Kutafakari kila swali, yaani kutafuta maana ya swali kwa kulihusisha na matini. e) Kujibu kila swali kwa kifupi na kwa usahihi. Dhana ya ufupisho wa habari Ufupisho wa habari ni kitendo au hali ya kupunguza maelezo ya habari ndefu uliyopewa na kuifanya kuwa fupi bila kupoteza maana yake ya msingi au maana ya awali. Jukumu la

Tài liệu liên quan

x
Báo cáo lỗi download
Nội dung báo cáo



Chất lượng file Download bị lỗi:
Họ tên:
Email:
Bình luận
Trong quá trình tải gặp lỗi, sự cố,.. hoặc có thắc mắc gì vui lòng để lại bình luận dưới đây. Xin cảm ơn.