Nội dung text Kusikiliza Mazungumzo Topic 4 - WazaElimu.com.pdf
2 Mzungumzaji au msemaji au msikilizaji wote kwa pamoja hutakiwa kuzingatia ufasaha wa maneno yanayotolewa Kusikiliza mazungumzo changamani. Mazungumzochangamani ni mazungumzo yale yanayohusu masuala muhimu yanayozungumziwa katika mazungumzo.katika kusikiliza mazungumzo changamani, msikiliza anatakiwa awe na kalamu na karatasi,kompyuta,simu au tablet kwa ajili ya kuandika mambo hayo muhimu kutoka kwenye habari anayoisikiliza.ikumbukwe kuwa mazungumzo changamani ni yale mazungumzo marefu ambayo yanahitaji msikilizaji awe makini kuchambua ni kusikiliza mambo muhimu. Mfano wa mazungumzo changamani ni hotuba za viongozi , kampeni za siasa, risala na mazungumzo mengine yenye mada mchanganyiko, Kufupisha mazungumzo changamani. Ufupisho ni taaluma inayohusu upunguaji wa maneno katika habari au mazungumzo kwa kuzingatia maudhui ya habari au mazungumzo husika . upunguzaji huo huyaondoa au kuyajumuisha maneneo yenye dhana moja bila kuathiri ujumbe uliokusudiwa katika kufupisha mazungumzo changamani ,unapaswa kuzingatia yafuatayo ; Kufupisha mazungumzo yawe mafupi kuliko ya mwanzo Kubakiza maana ileile katika mazungumzo uliyofupisha,usiondoe maneno ya msingi Kuwa na mtiririko mzuri wa mazungumzo yako nay awe na mantiki Tumia maneno yako mwenyewe Zingatia kutokpunguza ujumbe wa mazungumzo Tafuta maneno mengine yanayoweza kutumika badala ya fungu Fulani la maneno. Kwa mfano “kaka wa mama yangu ni mgonjwa” inaweza kuwa mjomba ni mgonjwa. Hatua za kufuata katika kufupisha mazungumzo changamani Sikiliza mazungumzo au habari yote kwa makini Bainisha mawazo makuu kutoka kwenye habari au mazungumzo uliyoyasikiliza Mazungumzo au habari uliyoisikiliza ina lugha fasaha na mtiririko mzuri wa mawazo Hakikisha hujapunguza ujumbe wa mazungumzo Husianisha mazungumzo muhimu na mazungumzo ya awali kama yanaendana Kushiriki katika majadiliano ya muktadha mbalimbali. Majadiliano ni kitendo cha kupeana mawazo chanya baina ya watu au pande mbili au zaidi ili kufikia muafaka wenye manufaa kuhusu suala au jambo fulani.