Content text Lugha na Utamaduni - Topic 1 - WazaElimu.com.pdf
1 SURA YA KWANZA Lugha na Utamaduni Dhana ya Lugha Binadamu huwasiliana kwa kutumia lugha. Lugha ndicho chombo kikuu cha mawasiliano ya binadamu. Lugha ni miongoni mwa vitambulisho vya utamaduni wa jamii fulani. Jamii hutumia lugha kusalimiana, kupashana habari na kubadilisha mawazo. Ushirikiano baina ya mtu na mtu hutokana na matumizi ya lugha Kwa ujumla tunaweza kufasili lugha kwa kusema Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa zenye maana zilizokubaliwa na jamii ya watu ili ziweze kutumika katika mawasiliano yao. Ni muhimu kutambua kuwa lugha ni kwa ajili ya binadamu na wala si kwa wanyama. Wanyama, wadudu na ndege huweza kuwasiliana miongoni mwao lakini hawana lugha. Maana(fasili) ya lugha inapotajwa mambo yafuatayo huzingatiwa; (i) Mfumo maalumu (mpangilio) Lugha lazima iwe na mpangilio maalumu ambao huanzia katika kiwango kidogo kabisa hadi kufikia kiwango cha juu. (ii) Sauti za nasibu (sauti za bahati tu), Mara nyingi hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya jina la kitu na kile kinachotajwa (kitu)pia hakuna kikao maalum kilichokaa ili kuchagua maneno ya lugha husika na maana zake. (iii) Maana- Lugha lazima iwe na maana kwa jamii inayoitumia (iv) Binadamu (jamii) – Lugha ni mali ya binadamu, binadamu pekee ndiye hutumia lugha. (v) Mawasiliano – Lugha ni chombo cha kupashana habari Vipashio vya lugha Vipashio vya lugha ni vipengele ambavyo kwa pamoja huijenga lugha. Lugha huundwa na vipashio vikuu vinne ambavyo ni sauti, silabi, neno na sentensi. (a)Sauti Sauti ni sehemu ndogo sana ya neno ambayo haiwezi kugawanyika zaidi. Kila lugha ina vitamkwa (sauti) vyake. Sauti zinazotumika katika lugha ya Kichina zinatofautiana na sauti zinazotumika katika lugha nyingine kama vile Kiingereza, Kijerumani, Kiswahili na kadhalika.
2 Mfano a, b, c,d,e,f,gh,h,I,j,k,l,m,n,nk. Sauti za lugha ya Kiswahili hugawanyika katika aina mbili ambazo ni irabu na konsonanti. (i)Irabu/vokali(I) Irabu ni sauti ambazo wakati wa utamkaji wake huwa hakuna kizuizi katika mkondo wa hewa utokao mapafuni na kupitia mdomoni. Kuna irabu tano za Kiswahili ambazo ni a, e, i, o, u (ii)Konsonanti(k) Konsonanti ni sauti ambazo wakati wa utamkaji wake huwa na kizuizi katika mkondo wa hewa utokao mapafuni na kupitia mdomoni.Kuna konsonanti kumi na tisa(19) katika lugha ya kiswahili ambazo ni b,ch,d,f,g,h,j,k,l,m,n,p,r,s,t,v,w,y na z Katika lugha ya Kiswahili kwa mfano neno “anacheza” limejengwa kwa vitamkwa a/n/a/ch/e/z/a. Vitamkwa au vipande- sauti hivyo ndivyo vinavyounda maneno. Kumbuka kwamba mawasiliano ya kutumia ishara si lugha. Vilevile mawasiliano baina ya wanyama, ndege na wadudu hayawezi kuitwa lugha kwa sababu vitamkwa vyake haviwezi kujulikana wala kuleta maana. (b)Silabi Silabi ni kipashio kidogo kinachojenga lugha ambacho hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Silabi inapoungana na silabi nyingine huunda neno. Miundo ya silabi Silabi huweza kujitokeza katika miundo ifuatayo; Irabu pekee(I) Mfano; Oa, Ua.Hapa kuna silabi mbili kwa kila neno yaani o-a,u-a Konsonanti pekee(K) Mfano;M-toto,M-kungu Konsonanti na irabu (KI) Mfano; Baba, Karatasi.Hapa kuna ba-ba,ka-ra-ta-si Konsonanti, konsonanti na irabu (KKI) Mfano; Mwezi, Chafya.Hapa kuna mwe-zi,cha-fya. Konsonanti, konsonanti, konsonanti na irabu (KKKI)