PDF Google Drive Downloader v1.1


Report a problem

Content text Sarufi ya Kiswahili Topic 2 - WazaElimu.com.pdf


Kuna baadhi ya maneno yasopotamkwa kwa usahihi huweza kubadili maana na kupoteza maana. Mfano - “Thamani” badala ya “Samani” - “Dhamani” badala ya “Zamani” Sarufi maana (Semantiki) Tawi hili la sarufi hushughulikia maana mbalimbali za maneno au maana za tungo katika lugha. Tawi hili ndilo ambalo hutawala matawi mengine yote ya sarufi kwasababu maana ya neno au tungo hutegemea na matamshi, muundo wa sentensi au maumbo ya maneno. Kuna maneno au sentensi ambazo huwa na maana zaidi ya moja. Mfano wa maneno hayo ni kama vile: mbuzi, kiboko, paa, ua, shuka nk. MATAMSHI Ni jinsi ya kutamka maneno katika lugha yoyote ile. Matamshi sahihi ni utamkaji wa maneno kwa kuzingatia kanuni za sarufi ya lugha inayohusika. Mzungumzaji akikosea kutamka neno humfanya msikilizaji asielewe kabisa au aelewe tofauti na alichokikusudia mzungumzaji. Mfano katika lugha ya Kiswahili mtu akitamka, “kura” badala ya “kula” itawasilisha maana tofauti na ilivyokusudiwa, hivyo hukwamisha mawasiliano. Katika lugha ya Kiswahili kuna vipengele vitatu muhimu vinavyozingatiwa katika matamshi. Vipengele hivyo ni lafudhi, kiimbo na mkazo. 1. Lafudhi Ni namna ya uzungumzaji au usemaji unaoipa utambulisho jamii fulani kutokana na lugha yao ya kwanza. Lafudhi ya mtu pia huweza kutokana na athari za jamii inayomzunguka hata kama jamii hiyo haizungumzi lugha yake ya kwanza. Hivyo lafudhi hutambulisha jamii au eneo analotoka mzungumzaji kama vile Mara, Kigoma, Rukwa, Mtwara, Singida, Pemba au Mbeya. Mifano ya lafudhi: ➢ Fiatu fyake fimechanika ( Wanyakyusa) ➢ Ntoto wako nchumbufu chacha ( Wamakonde) ➢ Mtoto amekura kisha akarara ( Wakurya) 2. Kiimbo Ni upandaji na ushukaji wa mawimbisauti wakati wa utamkaji au uimbikaji. Kila lugha ina utaratibu wake maalumu wa upandaji na ushukaji wa mawimbisauti katika utamkaji wake. Kuna aina nne za kiimbo ambazo ni: kiimbo cha maelezo, kiimbo cha swali, kiimbo cha amri na kiimbo cha mshangao. 2

Hivyo maana ya neno hili hutofautiana kwa kuweka mkazo wakati wa utamkwaji wake. Neno hili likitamkwa kwa kuwekwa mkazo litakuwa na maana ya sawasawa lakini likitamkwa bila kuwekwa mkazo litakuwa na maana ya njia. HERUFI/ SAUTI ZA KISWAHILI Herufi ni vitamkwa vya msingi sana katika lugha ambavyo huweza kufanya mtumiaji wa lugha kutamka au kuongea. Binadamu yeyote anaetumia lugha lazima ahusishe herufi na kinyume chake haiwezi kuwa lugha. Herufi hizi hutamkwa kwa kutumia ala sauti mfano mapafu, midomo, kaakaa gumu, meno nk. Herufi za Kiswahili hutamkwa kwa kuhusisha herufi husika na irabu /e / ambayo hupachikwa mbele ya herufi hiyo. Hata hivyo herufi ambayo ni irabu hutamkwa kama inavyoandikwa. Herufi za alfabeti Matamshi ya herufi A A B Be Ch Che D De Dh Dhe E E F Fe G Ge Gh Ghe H He I I J Je K Ke L Le M Me N Ne Ny Nye ng’ ng’e O O 4

Related document

x
Report download errors
Report content



Download file quality is faulty:
Full name:
Email:
Comment
If you encounter an error, problem, .. or have any questions during the download process, please leave a comment below. Thank you.