PDF Google Drive Downloader v1.1


Report a problem

Content text Kuwasiliana kwa njia ya maandishi Topic 7 - WazaElimu.com.pdf

1 SURA YA SABA Kuwasiliana kwa njia ya maandishi Dhana ya mawasiliano kwa njia ya maandishi Mawasiliano kwa njia ya maandishi ni aina ya mawasiliano ambayo huhusisha matumizi ya matini mbalimbali kama vile barua, hotuba, risala, kumbukumbu za vikao, kifungu cha habari na insha. Mambo yakuzingatia katika kufikisha ujmbe wa maandishi i. Mwandishi anapaswa kuzingatia ufasaha wa lugha anayotumia ili msomajia aweze kuelewa ujumbe uliokusudiwa ii. Mwandishi anapaswa kuzingatia matumizi ya lugha fasaha kwani yatamsaidia msomaji kuuelewa na kukuza lugha inayohusika kwa ufasaha iii. Mwandishi anapaswa kutumia msamiati sahihi unaoendana na muktadha wa mada inayohusika iv. Mwandishi anapaswa kuzingatia uhusiano sahihi wa maneno ili kujenga sentesi zinazoeleweka kwa msomaji v. Mwandishi anapaswa kuzingatia matumizi sahihi ya viunganishi na tahajia vi. Mwandishi anapaswa kuzingatia alama za uandishi vyema ili maudhui yaliyokusudiwa yaweze kumfikia msomaji. Taratibu za Uandishi Taratibu za uandishi ni alama na mpangilio wa maneno yanayo mwongoza mwandishi kuandika kwa usahihi. Ili habari iweze kuwa nzuri, inayoeleweka vizuri kwa wasomaji, mwandishi hana budi kutumia alama. Alama hizi humsaidia msomaji kujua wapi pa kupumzika, kuuliza swali, kushangaa, n.k. Alama zifuatazo hutumiwa katika uandishi: Nukta (.) (a) Hutumika kukamilisha sentensi Mfano:Mama anapika jikoni. (b) Hutumika kuonesha ufupisho wa maneno


Related document

x
Report download errors
Report content



Download file quality is faulty:
Full name:
Email:
Comment
If you encounter an error, problem, .. or have any questions during the download process, please leave a comment below. Thank you.